Page 22 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 22
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 2: Uhusiano wa fasihi simulizi na fasihi andishi
Shughuli ya 2.16
FOR ONLINE READING ONLY
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi ili kutumia vyanzo
vya maktabani na mtandaoni kujadili shughuli ya 2.16 iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha wawasilishe darasani.
Zingatia ushiriki wa kila mwanafunzi katika uwasilishaji wa
kazi za vikundi.
(ii) Waongoze wanafunzi kurekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa uwasilishaji ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.16 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano uhusiano wa fasihi
simulizi na fasihi andishi.
Somo la 3: Mchango wa fasihi simulizi katika fasihi andishi
Shughuli ya 2.17
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kutumia vyanzo
vya maktabani na mtandaoni kujadili shughuli ya 2.17 iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha wawasilishe darasani.
Zingatia ushiriki wa kila mwanafunzi katika uwasilishaji wa
kazi za vikundi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kufanya mdahalo unaohusu umuhimu wa
fasihi simulizi katika maendeleo ya fasihi andishi, kisha fanya
hitimisho la mdahalo huo.
16 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 16
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 16 23/06/2024 17:48