Page 26 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 26

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari





               Sura ya

                 Tatu                Kutathmini kazi za fasihi
           FOR ONLINE READING ONLY




                         Utangulizi

            Katika sura hii, mwanafunzi atajifunza kuhusu mitazamo, uhusiano
            na umuhimu wa vipengele vya fani na maudhui katika kazi za fasihi.
            Pia, atajifunza nadharia za uchambuzi wa kazi za fasihi pamoja na
            kuzitumia katika kuchambua kazi mbalimbali za kifasihi. Baada ya
            kujifunza ataweza kukuza stadi za uandishi na uchambuzi wa kazi za
            kifasihi. Mwalimu utapata baadhi ya mbinu zilizopendekezwa ambazo
            zitakuwezesha katika ujenzi wa umahiri huu kwa mwanafunzi. Hata
            hivyo,  unashauriwa kutumia  mbinu nyingine  utakazoona zinafaa
            kulingana na mazingira yako ili kukamilisha shughuli husika.





                             Shughuli za kutendwa na mwanafunzi



               (a)  Kujadili mitazamo inayohusu fani na maudhui;
               (b)  Kuhusianisha fani na maudhui katika kazi za fasihi;

               (c)  Kueleza umuhimu wa vipengele vya fani na maudhui katika
                    kazi za fasihi;

               (d)  Kuchambua nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi;
               (e)  Kuhakiki  kazi  za  fasihi  kwa kutumia  misingi  na  nadharia
                    mbalimbali; na

               (f)  Kutathmini mchango wa nadharia za uhakiki katika maende-
                    leo ya ushairi na tamthiliya.

             20                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   20    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   20
   21   22   23   24   25   26   27   28   29   30   31