Page 29 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 29
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.2(b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi achambue uhusiano uliopo
kwenye vipengele vya fani na maudhui kwa kutumia mifano ya kazi
FOR ONLINE READING ONLY
aliyoichambua.
Somo la 3: Umuhimu wa vipengele vya fani na maudhui katika
kazi za fasihi
Shughuli ya 3.3
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili
shughuli ya 3.3 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
kisha wawasilishe darasani kwa mjadala zaidi. Hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kwa kuchangia hoja wakati wa
uwasilishaji.
(ii) Washirikishe wanafunzi kurekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa uwasilishaji ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.3 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano umuhimu
wa fani na maudhui katika kazi fasihi.
(iii) Waongoze wanafunzi kukaa katika jozi na kufanya zoezi la 3.1
lililomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kusanya kazi
zao, sahihisha na toa mrejesho wa kazi zao.
Majibu
Majibu ya zoezi la 3.1 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Mwalimu
zingatia namna mwanafunzi anavyohusisha maarifa na maisha ya
Kiongozi cha Mwalimu 23
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 23 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 23