Page 32 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 32
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(iii) Waongoze wanafunzi kurekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa uwasilishaji.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 3.6 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze maana na misingi ya nadharia
ya umuundo katika kuhakiki kazi ya kifasihi.
Shughuli ya 3.7
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kuchunguza ramani ya dhana kuhusiana
na nadharia ya umaksi, kisha kwa njia ya maswali na majibu,
wafafanue maana na misingi ya nadharia hiyo.
(ii) Rekebisha upungufu unaojitokeza katika majibu yao.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.7 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze maana na misingi ya nadharia
ya umaksi katika kuhakiki kazi za kifasihi.
Shughuli ya 3.8
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
ya 3.8 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kufanya
uwasilishaji, hakikisha kila mwanafunzi anashiriki katika
uwasilishaji. Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa
uwasilishaji.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.8 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze maana na misingi ya nadharia
ya ufeministi katika kuhakiki kazi za fasihi.
26 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 26
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 26 23/06/2024 17:48