Page 37 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 37
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 3.15 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kughani au kusoma shairi lililopo
FOR ONLINE READING ONLY
kwenye shughuli ya 3.15(b), kisha kufanya shughuli binafsi ya
3.15 (b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu na kuchukua nukuu.
Kusanya kazi zao, sahihisha na kutoa mrejesho kwa wakati.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.15 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli 3.15 (b), mwanafunzi ahakiki shairi kwa kutumia
nadharia ya ufeministi kwa kuongozwa na maswali yaliyotolewa
Shughuli ya 3.16
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma matini fupi ya tamthiliya iliyomo
katika shughuli ya 3.16 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi
huku wakiandika dondoo muhimu, kisha kufanya uwasilishaji.
Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki katika uwasilishaji.
(ii) Waongoze wanafunzi kuhusianisha misingi ya nadharia ya
umaksi na dondoo mbalimbali walizozichukua wakati wa
uchambuzi wa matini hiyo.
(iii) Rekebisha upungufu unaojitokeza katika majibu watakayoyatoa.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.16 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua matini fupi ya tamthiliya
kwa kutumia misingi ya nadharia ya umaksi.
Kiongozi cha Mwalimu 31
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 31 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 31