Page 41 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 41
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 4.2 (a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mkondoni kupakua
FOR ONLINE READING ONLY
na kusikiliza wimbo wowote wa bongo fleva unaosawiri
umuhimu wa wazazi, kisha kila mwanafunzi ajibu maswali
yaliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kuandaa uwasilishaji. Chagua baadhi ya
wanafunzi wawasilishe kazi zao darasani kwa majadiliano huku
ukirekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
(iii) Waongoze wanafunzi kuhitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla
kuhusu shughuli husika.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.2 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili kwa kuongozwa
na maswali yaliyotolewa. Mwanafunzi atumie mifano kutoka kwenye
wimbo husika na kuhusianisha hoja zake na maisha halisi.
Shughuli ya 4.2(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vifaa vya TEHAMA kupakua na
kusikiliza nyimbo za bongo fleva.
(ii) Waongoze wanafunzi kukaa katika jozi na kila jozi ichambue
maadili ya wimbo mmojawapo kati ya walizozisiliza.
(iii) Waongoze wanafunzi kukusanya, sahihisha na toa mrejesho wa
kazi zao.
Kiongozi cha Mwalimu 35
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 35 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 35