Page 36 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 36

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


                  uwasilishaji.
             (ii)  Waongoze  wanafunzi  kuhusianisha  misingi  ya  nadharia  ya
                  uumundo wakati wa uchambuzi wa shairi hilo.

           FOR ONLINE READING ONLY
             (iii)  Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
           Majibu

           Majibu  ya  shughuli  ya  3.14  yatatokana  na  uelewa  wa  mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi ahakiki shairi kwa kutumia nadharia
           ya umuundo. Hakikisha mwanafunzi anatumia  misingi ya nadharia
           husika na mifano kutoka katika kazi teule ya kifasihi.

           Shughuli ya 3.15 (a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Unda jozi za wanafunzi, kisha waongoze kughani au kusoma
                  shairi  lililomo  katika  shughuli  ya  3.15  (a)  kwenye  Kitabu
                  cha  Mwanafunzi  kwa kupokezana,  huku wakiandika  nukuu
                  muhimu.

             (ii)  Waongoze wanafunzi kuchambua shairi kwa kutumia maswali
                  ya mwongozo yaliyowekwa baada ya shairi hilo.

             (iii)  Kwa njia  ya maswali  na majibu,  waongoze wanafunzi
                  kuwasilisha uchambuzi  walioufanya  kwa kuhusanisha na
                  misingi ya nadharia ya umuundo.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 3.15 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika  shughuli  3.15 (a) iliyomo  kwenye Kitabu  cha Mwanafunzi,
           hakikisha mwanafunzi anahakiki mashairi mawili kutoka katika diwani
           teule kwa kutumia nadharia ya umuundo.







             30                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   30    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   30
   31   32   33   34   35   36   37   38   39   40   41