Page 35 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 35
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 6: Kuhahiki maigizo mashairi na tamthiliya kwa
kutumia nadharia za kifashi
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 3.13
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutazama au kusikiliza maigizo kwa
kutumia vifaa vya TEHAMA, mwanafunzi anaweza kusikiliza
au kutazama akiwa nyumbani au shuleni kulingana na mazingira
yake huku akinukuu dondoo muhimu kuhusiana na maswali ya
mwongozo yaliyomo katika shughuli ya 3.13(a) na (b) i - v.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
ya 3.13(a) na (b) zilizopo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
kisha kufanya uwasilishaji. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki katika uwasilishaji.
(iii) Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.13 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli 3.13(a) mwanafunzi ahakiki igizo kwa kutumia nadharia
ya uhalisia. Katika shughuli 3.13(b), mwanafunzi atumie nadharia ya
mwitiko wa msomaji katika kuhakiki maigizo matatu aliyoyatazama
au kuyasikiliza. Hakikisha mwanafunzi anatumia misingi ya nadharia
husika kwa kuongozwa na maswali i – v yaliyotolewa.
Shughuli ya 3.14
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma shairi lililomo katika shughuli ya
3.14 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi huku wakinukuu
dondoo muhimu wakati wa uchambuzi, kisha kufanya
uwasilishaji. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki katika
Kiongozi cha Mwalimu 29
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 29 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 29