Page 39 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 39
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Sura ya
Nne Maadili katika fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Katika sura hii, mwanafunzi atajifunza maadili yaliyomo katika
nyimbo za bongo fleva, mashairi na tamthiliya. Pia, atajifunza
misingi ya maadili, umuhimu wa maadili katika jamii, ulinganisho
wa maadili yaliyomo katika kazi za fasihi. Vilevile, atajifunza namna
ya kueleza na kuhusianisha mitazamo iliyomo katika kazi hizo za
fasihi na matendo ya jamii. Kadhalika, atajifunza athari za kiimani
na kimtazamo zinavyojidhihirisha katika kazi za kifasihi. Hata hivyo,
baadhi ya mbinu zimependekezwa katika hatua za ufundishaji lakini
unashauriwa kutumia mbinu nyinginezo zitakazowezesha katika
ujenzi wa umahiri kwa mwanafunzi. Baada ya kujifunza, ataweza
kutunga kazi za fasihi zenye maadili kulingana na imani za jamii
husika.
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kueleza maadili yaliyomo katika nyimbo za bongo fleva,
mashairi na tamthiliya;
(b) Kulinganisha maadili yaliyomo katika bongo fleva, mashairi,
tamthiliya na imani za jamii ;
(c) Kueleza mitazamo iliyomo katika bongo fleva, mashairi na
tamthiliya ;
Kiongozi cha Mwalimu 33
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 33 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 33