Page 42 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 42
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.2 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili kwa kuongozwa
na maswali yaliyotolewa.
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 4.3(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kughani au kusoma shairi lililomo katika
shughuli ya 4.3 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Kwa njia ya maswali na majibu, waongoze wanafunzi kujibu
maswali yaliyopo baada ya shairi.
(iii) Waelekeze wanafunzi kuchambua maadili kisha kukusanya
kazi zao. Sahihisha na toa mrejesho wa shughuli hiyo kwa
wanafunzi wote.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.3 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili yaliyomo
katika shairi kwa kuongozwa na maswali yaliyomo katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
Shughuli ya 4.3(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.3 (b) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika kikundi cha wanafunzi
wasiozidi wanne, kisha wachambue maadili yaliyomo katika
mashairi mawili kutoka kwenye diwani teule.
36 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 36
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 36 23/06/2024 17:48