Page 46 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 46
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.6 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hizi, mwanafunzi atachambua maadili kwa
kuyalinganisha na masuala ya kiimani yaliyomo katika kazi hizo. Ili
FOR ONLINE READING ONLY
kufanya shughuli hizi kwa ufanisi, mwanafunzi anapaswa kuyafahamu
vizuri maadili na imani za jamii yake.
Shughuli ya 4.6 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.6 (a) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi ili kupakua na
kusikiliza nyimbo za bongo fleva, kisha kuchambua maadili
yaliyomo katika nyimbo hizo.
(iii) Teua wanafunzi wachache, kisha waongoze kuwasilisha kwa
niaba ya wengine. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
kikamilifu wakati wa uwasilishaji. Rekebisha upungufu
unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
Shughuli ya 4.7(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kughani au kusoma
shairi lililomo katika shughuli ya 4.7(a) iliyomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kujadiliana katika jozi, shughuli ya 4.7(a)
iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha teua baadhi ya
jozi ziwasilishe darasani. Rekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa uwasilishaji.
40 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 40 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 40