Page 49 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 49

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari




             Somo la 3:  Mitazamo iliyomo katika bongo fleva, mashairi na
                        tamthiliya

           FOR ONLINE READING ONLY
           Shughuli ya 4.9 (a)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kwa njia ya maswali na majibu kubainisha
                  mitazamo iliyomo katika jamii.

             (ii)  Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandaoni au
                  vinginevyo  kusikiliza  au  kutazama  wimbo  wa  bongo  fleva
                  unaosawiri  athari  za  starehe  kisha  kukaa  katika vikundi
                  visivyozidi wanafunzi watano kujadiliana kuhusu shughuli ya
                  4.9(a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kuwasilisha, unaweza kuchagua baadhi
                  ya vikundi kuwasilisha kwa niaba ya vikundi vingine. Sisitiza
                  ushiriki wa kila mwanafunzi kwa kuchangia mawazo wakati
                  wa uwasilishaji.

             (iv)  Rekebisha upungufu unaojitokeza  wakati wa uwasilishaji ili
                  kuleta uelewa wa pamoja.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.9 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo kwa kuongozwa
           na maswali yaliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi.

           Shughuli ya 4.9(b)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waelekeze  wanafunzi kupakua na kusikiliza  au kutazama
                  nyimbo  mbili  za  bongo  fleva,  kisha  kuchambua  mitazamo




                 Kiongozi cha Mwalimu                                    43
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   43    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   43
   44   45   46   47   48   49   50   51   52   53   54