Page 53 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 53
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
jozi, kisha kufanya shughuli ya 4.12 (b) iliyomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi. Katika majadiliano, kila mwanafunzi aandike
uchambuzi wake.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya kazi zao, sahihisha na toa
FOR ONLINE READING ONLY
mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.12 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha mitazamo
na matendo ya jamii kwenye wimbo mmoja wa bongo fleva.
Shughuli ya 4.13(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma au kughani shairi lililomo kwenye
shughuli ya 4.13 kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kukaa
katika jozi na kuchambua uhusiano wa mitazamo na matendo
ya jamii kwa kuongozwa na maswali yaliyomo katika shughuli
ya 4.13 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kuwasilisha darasani shughuli
waliyoifanya. Hakikisha ushiriki wa kila jozi wakati wa
uwasilishaji ili kupata mawazo ya kila mmoja. Rekebisha
upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji
(iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
waliyoiwasilisha
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.13 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua shairi na kuhusianisha
mitazamo na matendo ya jamii kwa kuongozwa na maswali yaliyotolewa.
Kiongozi cha Mwalimu 47
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 47 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 47