Page 51 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 51
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.10 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo iliyomo katika
mashairi mawili atakayokuwa ameyachambua kutoka katika diwani
FOR ONLINE READING ONLY
teule.
Shughuli ya 4.11(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma kipande cha tamthiliya
kilichomo katika shughuli ya 4.11(a) iliyomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi, kisha wajibu maswali yanayofuata baada ya
kipande hicho.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya kazi zao kisha sahihisha na
toa mrejesho darasani.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.11(a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo kutoka kwenye
kipande cha tamthiliya alichokisoma kwa kuongozwa na maswali
aliyopewa.
Shughuli ya 4.11(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi kuchambua shughuli
ya 4.11(b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
kuwasilisha darasani kwa majadiliano zaidi.
(ii) Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji huo.
Kiongozi cha Mwalimu 45
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 45 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 45