Page 54 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 54
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 4.13(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Unaweza kutumia mbinu ya changanya kete kuwaongoza
FOR ONLINE READING ONLY
wanafunzi kuhusisha mitazamo ya jamii na mawazo yaliyomo
katika mashairi mbalimbali yaliyomo kwenye diwani teule.
(ii) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kuchambua shughuli
ya 4.13 (b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
wakusanye kazi zao. Sahihisha na toa mrejesho kwa wanafunzi.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.13 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha matendo
ya jamii na mitazamo iliyomo kwenye mashairi mawili ya diwani teule.
Shughuli ya 4.14(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma kipande cha tamthiliya kilichomo
katika shughuli 4.14(a) kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
kukaa katika vikundi ili kuhusisha mitazamo ya jamii na
mawazo yaliyomo kwenye kipande cha tamthiliya.
(ii) Waongoze wanafunzi kuwasilisha darasani kazi walizozifanya
katika vikundi vyao kwa majadiliano zaidi huku ukirekebisha
upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.14 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha mitazamo
na matendo ya jamii kwa kujibu maswali yaliyotolewa.
48 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 48 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 48