Page 57 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 57

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.16 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli 4.16 (a), mwanafunzi atachambua athari za kiimani na
           FOR ONLINE READING ONLY
           mitazamo katika nyimbo kwa kujibu maswali yaliyotolewa.
           Shughuli ya 4.16(b)

           Hatua za ufundishaji

              (i)  Waongoze wanafunzi kusoma na kuchambua mashairi mawili
                  kutoka katika diwani teule, kisha kukaa katika jozi na kujadili
                  shughuli ya 4.16 (b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

              (ii) Waelekeze wanafunzi kufanya uwasilishaji, chagua wanafunzi

                  wachache  kuwasilisha kazi zao darasani kwa majadiliano zaidi
                  huku ukirekebisha upungufu unaojitokeza.

              (iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
                  husika.


           Majibu
           Majibu ya shughuli ya 4.16 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli 4.16 (b), mwanafunzi atachambua athari za kiimani na
           mitazamo katika mashairi mawili kutoka kwenye diwani teule.

           Shughuli ya 4.17(a)

           Hatua za ufundishaji

              (i)  Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kusoma matini
                  fupi ya tamthiliya iliyomo katika shughuli ya 4.17 (a) katika
                  Kitabu cha Mwanafunzi.
              (ii) Waongoze wanafunzi kuwasilisha kazi zao darasani kwa

                  majadiliano  zaidi huku ukirekebisha upungufu unaojitokeza


                 Kiongozi cha Mwalimu                                    51
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   51    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   51
   52   53   54   55   56   57   58   59   60   61   62