Page 62 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 62
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(ii) Waongoze wanafunzi kuchambua diwani teule kwa kutumia
misingi ya ujumi. Ongoza mjadala, kisha rekebisha upungufu
unaojitokeza.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 5.2 (c) yatategemea uelewa wa mwanafunzi na
diwani teule atakazozitumia mwanafunzi katika uchambuzi. Katika
uchambuzi, mwanafunzi azingatie misingi ya ujumi ili kuitumia
kuhakiki diwani teule.
Somo la 2: Mbinu zinazotumika kujenga ujumi katika kazi za
fasihi
Shughuli ya 5.3 (a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.3(a) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Ongoza mjadala kisha
rekebisha upungufu unaojitokeza.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi na kujadili shughuli
ya 5.3 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
uliza maswali yanayowafikirisha wanafunzi. Hakikisha kila
mwanafunzi anatoa mawazo yake. Rekebisha dosari pale
zinapojitokeza.
(iii) Waongoze wanafunzi kuandaa uwasilishaji, chagua vikundi
vichache ili kuwakilisha vingine. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki kwa kutoa mchango au kuuliza maswali. Sahihisha
upungufu unaojitokeza, kisha toa mrejesho wa shughuli husika.
56 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 56 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 56