Page 66 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 66
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(ii) Waongoze wanafunzi kusoma shairi lililomo katika shughuli
ya 5.6 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
jibu maswali yanayotokana na shairi hilo. Hakikisha kila
mwanafunzi anasoma na kujibu maswali hayo. Rekebisha
FOR ONLINE READING ONLY
dosari pale zitakapojitokeza.
(iii) Waelekeze wanafunzi kuandaa uwasilishaji, chagua wanafunzi
wachache kujibu swali mojamoja kama alivyolichambua na
kuwasilisha kwa darasa zima. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki kwa kutoa mchango au kuuliza maswali. Sahihisha
upungufu unaojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.6 (a) yatategemea uelewa wa mwanafunzi na
mashairi atakayoyachambua kutoka katika diwani teule. Mwanafunzi
achambue maana mbalimbali kwa kujibu maswali aliyopewa kwa
kutumia mifano kutoka katika mashairi husika.
Shughuli ya 5.6 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kuchambua mashairi mawili kutoka
katika diwani teule. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
kikamilifu katika uchambuzi na kuchukua nukuu.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya kazi. Sahihisha kazi hizo,
kisha toa mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.6 (b) yatategemea uelewa wa mwanafunzi
na mashairi atakayoyachambua kutoka katika diwani teule. Katika
kuchambua maana, mwanafunzi atumie mifano kutoka mashairi husika.
60 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 60
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 60 23/06/2024 17:48