Page 70 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 70
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 5: Misingi ya ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi
Shughuli ya 5.10
FOR ONLINE READING ONLY
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.10 iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kukusanya mazungumzo ya makundi
mawili (mtoto au watoto wadogo wenye umri wa kuanza shule
na kiongozi yeyote wa serikali).
(iii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi viwili, kila kikundi
kichukue aina moja ya mazungumzo na kujadili aina, maana na
mpangilio wake wa hoja. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
kikamilifu. Rekebisha dosari zinazojitokeza.
(iv) Waongoze wanafunzi kuandaa uwasilishaji kuhusu
mazungumzo, kila kikundi kiwasilishe hoja zake. Hakikisha kila
mwanafunzi anashiriki kwa kutoa mchango au kuuliza maswali
ili kuendeleza mjadala. Sahihisha upungufu unaojitokeza katika
uwasilishaji, kisha toa mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli 5.10 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi ataeleza aina, maana na mpangilio wa hoja
zinazotolewa katika mazungumzo wa kila kundi.
Shughuli ya 5.11 (a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.11(a) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
64 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 64
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 64 23/06/2024 17:48