Page 72 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 72

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 5.12 (a)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kufanya shughuli ya 5.12 (a) iliyomo
           FOR ONLINE READING ONLY
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi ili kujenga hoja zenye mantiki
                  na ushawishi kuhusu ujenzi wa wahusika.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kuigiza kipande cha dailojia ya usaili, wa
                  kisha chambua hoja zenye mantiki na ushawishi kuhusu ujenzi
                  wa wahusika wake. Hakikisha  kila  mwanafunzi  anashiriki
                  kikamilifu katika kuigiza na kujibu maswali kwa kutoa  mifano
                  maridhawa.  Katika uchambuzi, wanafunzi waongozwe na
                  maswali yaliyotolewa. Rekebisha dosari zinazojitokeza.

             (iii)  Waelekeze  wanafunzi  kuandaa  uwasilishaji,  kisha chagua
                  wanafunzi  wachache  wawasilishe  kazi  zao.  Hakikisha kila
                  mwanafunzi anashiriki kwa kutoa mchango au kuuliza maswali.
                  Sahihisha upungufu unaojitokeza katika uwasilishaji, kisha toa
                  mrejesho.

           Majibu

           Majibu ya shughuli 5.12 (a) yatatokana  na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atajibu kwa kuongozwa na maswali
           yaliyotolewa katika ujenzi wa hoja zenye ushawishi na mantiki katika
           mchakato wa usaili.

           Shughuli ya 5.12 (b)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kuandaa usaili ambao unawasilisha
                  hoja zenye mantiki na ushawishi katika nafasi ya kazi ambayo
                  mwanafunzi ataichagua. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
                  kikamilifu  katika  kuandaa  usaili  wa kazi  atakayoichagua  na
                  kuchukua nukuu.



             66                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   66
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   66    23/06/2024   17:48
   67   68   69   70   71   72   73   74   75   76   77