Page 68 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 68

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari



             Somo la 4:  Mbinu za kifasihi zinavyoathiri kupatikana  kwa
                        maana katika kazi za kifasihi


           FOR ONLINE READING ONLY
           Shughuli ya 5.8 (a)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.8 (a) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi kukaa katika  vikundi na kujadili
                  shughuli ya 5.8 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
                  kisha uliza maswali yanayowafikirisha wanafunzi. Hakikisha
                  kila  mwanafunzi  anatoa  mawazo  yake. Rekebisha dosari
                  zinazojitokeza.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kuwasilisha ambapo, kila kikundi kitajibu
                  swali moja. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kwa kutoa
                  mchango au kuuliza maswali ili kuendeleza mjadala. Sahihisha
                  upungufu unaojitokeza katika uwasilishaji, kisha toa mrejesho
                  wa shughuli husika.
           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 5.8 (a) yatategemea uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, atachambua maana mbalimbali kutoka katika shairi
           husika.

           Shughuli ya 5.8 (b)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Muongoze  kila  mwanafunzi  kufanya  shughuli  5.8  (b)  kwa
                  kuchambua shairi moja kutoka katika diwani teule. Hakikisha
                  kila  mwanafunzi  anashiriki  kikamilifu  katika  uchambuzi  na
                  kuchukua nukuu.



             62                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   62    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   62
   63   64   65   66   67   68   69   70   71   72   73