Page 71 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 71
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(ii) Waongoze wanafunzi kuchambua hoja zenye mantiki na
ushawishi kuhusu ujenzi wa wahusika kutoka katika kipande cha
tamthiliya. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu.
Rekebisha dosari zinazojitokeza.
FOR ONLINE READING ONLY
(iii) Waelekeze wanafunzi kuandaa uwasilishaji, chagua wanafunzi
wachache wawasilishe kazi zao. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki kwa kutoa mchango au kuuliza maswali. Sahihisha
upungufu unaojitokeza katika uwasilishaji, kisha toa mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.11 (a) yatategemea uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli ya hii mwanafunzi aoneshe namna alivyotumia misingi
ya ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi katika kutathimini
matendo ya wahusika katika kipande cha tamthiliya.
Shughuli ya 5.11(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kuchambua namna misingi ya ujenzi
wa hoja zenye mantiki na ushawishi katika kutathimini
matendo ya wahusika katika tamthiliya mbili teule. Hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika uchambuzi na
kuchukua nukuu.
(ii) Kusanya na kusahihisha kazi za wanafunzi ili kuondoa upungufu
unaojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.11 (b) yatategemea uelewa wa mwanafunzi na
tamthiliya teule atakayoichambua. Pia shughuli ya 5.11 (b) yatatokana
na tamthiliya teule atakayoichambua mwanafunzi. Katika uchambuzi
mwanafunzi aoneshe namna alivyotumia misingi ya ujenzi wa hoja
zenye mantiki na ushawishi katika kutathimini matendo ya wahusika
katika tamthiliya mbili teule.
Kiongozi cha Mwalimu 65
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 65 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 65