Page 74 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 74

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi vinne, kila kikundi
                  kichague  mada  moja  kati  ya  hizo  zilizoorodheshwa kwenye
                  Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kutunga malumbano ya hoja
                  kwa kutumia  maarifa  ya kifasihi  ili  kuwasilisha hoja zenye
           FOR ONLINE READING ONLY
                  mantiki  na ushawishi. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
                  kikamilifu. Rekebisha dosari zinazojitokeza.

             (iii)  Waongoze  wanafunzi  kuandaa  uwasilishaji.  Kila kikundi
                  kiwasilishe malumbano  ya hoja kulingana  na mada
                  waliyopangiwa.  Hakikisha kila  mwanafunzi  anashiriki kwa
                  kutoa maoni au kuuliza maswali ili kuboresha kazi ya kikundi
                  husika.  Sahihisha  upungufu  unaojitokeza  katika  uwasilishaji,
                  kisha toa mrejesho.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 5.13 yatategemea uelewa wa mwanafunzi kwa
           kuzingatia  mada aliyoichagua.  Katika utunzi wa malumbano  hayo,
           mwanafunzi  aoneshe namna  anyowasilisha  hoja zenye  mantiki  na
           ushawishi.

           Shughuli ya 5.14

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.14 iliyomo kwenye
                  Kitabu cha Mwanafunzi.
             (ii)  Waongoze  wanafunzi  kuchagua  mada  yoyote  anayoipenda,
                  kisha kutunga malumbano  ya hoja kwa kutumia  maarifa  ya
                  kifasihi  ili  kuwasilisha  hoja  zenye  mantiki  na  ushawishi.
                  Hakikisha  kila  mwanafunzi  anashiriki  kikamilifu.  Rekebisha
                  dosari zinazojitokeza.

             (iii)  Kusanya na sahihisha kazi za wanafunzi ili kuondoa upungufu
                  unaojitokeza.




             68                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   68    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   68
   69   70   71   72   73   74   75   76   77   78   79