Page 77 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 77

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


               (f)  Kuchambua kanuni za utunzi na kutunga mashairi; na
               (g)  Kuchambua kanuni za utunzi na kutunga na hadithi za watoto.

           Mahitaji
           FOR ONLINE READING ONLY
           Matini  na  makala  za  kifasihi, kamusi, magazeti,  hadithi,  nyimbo,
           mashairi na maigizo yaliyorekodiwa.



             Somo la 1: Miktadha inayochagiza utunzi wa kazi za fasihi

           Shughuli ya 6.1 (a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Kwa njia ya maswali na majibu waongoze wanafunzi kuibua
                  masuala yanayohusiana na utunzi wa kazi za kifasihi.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
                  ya 6.1(a) iliyomo  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
                  kuwasilisha hoja zao kwa ajili ya majadiliano zaidi.

           Majibu
           Majibu ya shughuli ya 6.1 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika  shughuli  6.1 (a), mwanafunzi  aeleze  miktadha inayochangia
           utunzi wa kazi za fasihi.

           Shughuli ya 6.1 (b)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waelekeze  wanafunzi  kukusanya kazi  mbalimbali  za  fasihi.
                  Kwa njia ya maswali na majibu, waongoze kuchambua kuwapo
                  tofauti mbalimbali za kuibuliwa kwa kazi hizo.

             (ii)  Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili
                  shughuli ya 6.1(b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
                  kisha kuwasilisha  hoja  zao kwa ajili  ya majadiliano zaidi.

                 Kiongozi cha Mwalimu                                    71
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   71    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   71
   72   73   74   75   76   77   78   79   80   81   82