Page 82 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 82
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(iii) Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa majadiliano na
uwasilishaji ili kuondoa dosari zinazojitokeza.
(iv) Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 6.2 lililomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi, kisha sahihisha na kuondoa makosa
FOR ONLINE READING ONLY
yatakayojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli 6.6 yanaweza kutokana na uelewa wa mwanafunzi.
Pamoja na yale yaliyopo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Pia, majibu
ya zoezi la 6.2 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi
Somo la 5: Kanuni za utunzi na kutunga maigizo
Shughuli ya 6.7 (a)
Hatua za ufundishaji
(i) Tumia njia ya bungua bongo kuwaongoza wanafunzi kueleza
tofauti kati ya hatua na kanuni za utunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 6.7 (a) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(iii) Waelekeze wanafunzi kuunda vikundi vitatu wakiwa darasani.
Kikundi cha kwanza kijadili kuhusu maana ya maigizo, kikundi
cha pili kijadili kuhusu kanuni za utunzi wa maigizo na kikundi
cha tatu kijadili kuhusu umuhimu wa maigizo. Hakikisha kila
mwanafunzi anashiriki katika kutoa mawazo yake. Tembelea
kila kikundi ili kurekebisha dosari zinazojitokeza katika
majadiliano.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji, kila kikundi
kichague mwakilishi awasilishe kazi yao na wanafunzi wengine
washiriki kuchangia hoja na kuuliza maswali. Rekebisha dosari
zinazojitokeza katika uwasilishaji.
76 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 76
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 76 23/06/2024 17:48