Page 87 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 87
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 6.12
Hatua za ufundishaji
(i) Andaa mazingira ya kufanyika kwa shindano la utunzi wa
FOR ONLINE READING ONLY
hadithi za watoto.
(ii) Waongoze wanafunzi kutunga hadithi za watoto. Kila
mwanafunzi achague mada moja kati ya zile zilizobainishwa
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Kuweka vigezo vya ushindani
kwa kuzingatia hatua na kanuni za utunzi wa hadithi za watoto.
Unaweza kufuata hatua zifuatazo:
• Kutoa muda wa utungaji unaweza kuwa wiki mbili hadi
tatu;
• Kukusanya hadithi hizo;
• Kuandaa jopo la majaji watakaotathmini kazi hizo
(wanaweza kuwa walimu, wanafunzi wenzao au wataalamu
wengine wa fasihi);
• Kuandaa na kupitia vigezo vya kutathmini hadithi hizo;
• Kuanza mchakato wa kutathmini; na
• Kutangaza washindi.
(iii) Waelekeze wanafunzi kufanya tamrini iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi, kisha sahihisha na kuondoa makosa
yanayoweza kujitokeza.
Majibu
Majibu ya tamrini yatategemeana na uelewa wa mwanafunzi. Pia,
unaweza kupima namna mwanafunzi anavyoweza kuhawilisha maarifa
na kuyaweka katika mazingira na maisha halisi.
Kiongozi cha Mwalimu 81
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 81 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 81