Page 85 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 85

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Majibu
           Majibu  ya shughuli ya 6.9 yatatokana na uelewa  wa mwanafunzi.
           Pia, yanaweza kuwa yale yaliyopo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
           Mwanafunzi  aeleze  namna anavyotumia  lugha  ya kishairi,  muundo,
           FOR ONLINE READING ONLY
           muwala, taswira na ishara, mtindo na utosherevu wa shairi kuanzia
           kwenye mshororo/mstari, kwenye ubeti na shairi zima. Mambo haya
           yabainishwe vizuri kishairi na namna yanavyotofautiana yanapotumika
           katika tanzu zingine.

           Shughuli ya 6.10 (a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kughani  au kusoma mashairi mawili
                  kutoka katika diwani teule, kisha wachambue kanuni
                  zilizotumika  katika  utunzi wa mashairi.  Hakikisha kila
                  mwanafunzi  anashiriki  kikamilifu  katika  uchambuzi  na
                  kuandika tini.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukusanya kazi, kisha sahihisha kazi za
                  wanafunzi ili kuondoa upungufu unaojitokeza.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 6.10 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi
           na diwani teule atakazozichambua.

           Shughuli ya 6.10 (b)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kufanya  shughuli  ya  6.10(b)  iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Kusanya kazi na sahihisha kisha toa mrejesho.






                 Kiongozi cha Mwalimu                                    79
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   79    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   79
   80   81   82   83   84   85   86   87   88