Page 83 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 83
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli 6.7 (a) yatatokana na mawazo wa mwanafunzi. Pia,
yanaweza kuwa yale yaliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 6.7 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 6.7 (b) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kupakua igizo lolote kwa kutumia
kifaa cha TEHAMA kinachopatikana katika mazingira ya
shuleni, kisha kuchambua kanuni zilizotumika katika utunzi
wa igizo hilo. Au waagize mwanafunzi kupakua na kutazama
au kusikiliza igizo lolote akiwa nyumbani, kisha wachambue
kanuni zilizotumika katika utunzi wa igizo husika.
(iii) Waongoze wanafunzi kuandaa uwasilishaji wa kanuni za utunzi
wa maigizo. Chagua wanafunzi wachache wawasilishe na
wengine wasikilize, huku wakichangia mawazo yao na kuuliza
maswali kuhusu kile kinachowasilishwa. Rekebisha dosari
zinazojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 6.7 (b) yatatokana na mawazo ya mwanafunzi.
Pia, yanaweza kuwa yale yaliyopo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
Katika kufanya shughuli hii, mwanafunzi abainishe wazi tofauti
zilizomo katika vipengele vya matumizi ya dayalojia, uumbaji wa visa
na vitendo, ujitokezaji wa migogoro, uumbaji wa wahusika, uchaguzi
wa mandhari na namna mtunzi anavyogusa hisia za hadhira katika
utunzi wa maigizo vinavyotofautiana na katika ushairi na hadithi za
watoto.
Kiongozi cha Mwalimu 77
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 77 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 77