Page 78 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 78
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Katika uwasilishaji waulize wanafunzi maswali kujua kama
wameelewa na sahihisha upungufu unaojitokeza.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 6.1 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi achambue miktadha iliyooibua kazi
alizozikusanya. Pia, unaweza kumrejesha mwanafunzi katika mazingira
yake ya kawaida kwa kumuuliza kama akitaka kutunga kazi ya fasihi
nini kitamsukuma na kuchochea uteuzi wa mada.
(i) Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 6.1 lililomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi, kisha sahihisha na kuondoa makosa
yanayojitokeza.
Somo la 2: Fursa mbalimbali zinazotokana na kazi za kifasihi
za Kiswahili
Shughuli ya 6.2
Hatua za ufundishaji
(i) Kwa njia ya bungua bongo, waongoze wanafunzi kutambua
dhana ya fursa katika muktadha wa kazi za fasihi.
(ii) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kujadili fursa
zinazotokana na kazi ya fasihi. Wanafunzi wabandike kazi
za kila kikundi kwenye ukuta wa darasa, kisha wanafunzi
wazitembelee na kuzisoma kwa kupokezana.
(iii) Waongoze wanafunzi kuuliza maswali ili kupima uelewa wa
wanafunzi na kutoa ufafanuzi kwenye hoja zinazowatatiza, kisha
toa ufupisho wa kile walichokuwa wakijadiliana wanafunzi.
72 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 72
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 72 23/06/2024 17:48