Page 76 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 76

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari





               Sura ya

                 Sita           Kubuni kazi changamani za fasihi
           FOR ONLINE READING ONLY





                         Utangulizi
            Katika sura hii, mwanafunzi atajifunza kuhusu miktadha inayochochea
            utunzi wa kazi changamani za fasihi; fursa zinazohusiana na utunzi
            na uchapishaji wa kazi za fasihi; na mchango wa TEHAMA katika
            kuongeza fursa zinazotokana na kazi za fasihi. Pia, atajifunza hatua,
            kanuni za utunzi, na kutunga kazi za fasihi simulizi na fasihi andishi.
            Umahiri utakaomjengea mwanafunzi utamwezesha kutunga maigizo,
            mashairi na hadithi za watoto na kuzitumia kazi hizo kama fursa
            ya kujiingizia kipato binafsi na jamii kwa ujumla. Mwalimu utapata
            mbinu na utaratibu utakaokuwezesha katika ujenzi wa umahiri huu
            kwa mwanafunzi.






                             Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


               (a)  Kueleza miktadha inayochagiza utunzi wa kazi za fasihi.

               (b)  Kufafanua fursa mbalimbali zinazotokana na kazi za kifasihi
                    za Kiswahili.

               (c)  Kueleza  mchango wa  TEHAMA katika kutambua fursa
                    zinazotokana na kazi za fasihi.

               (d)  Kufafanua hatua za utunzi wa kazi za kifasihi.
               (e)  Kuchambua kanuni za utunzi na kutunga maigizo.



             70                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   70
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   70    23/06/2024   17:48
   71   72   73   74   75   76   77   78   79   80   81