Page 73 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 73
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya na kusahihisha kazi za
wanafunzi ili kuondoa upungufu unaojitokeza.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 5.12 (b) yatategemea uelewa wa mwanafunzi
kwa kuzingatia nafasi ya kazi ambayo mwanafunzi ataichagua. Katika
uchambuzi, mwanafunzi aoneshe namna atakavyowasilisha hoja zenye
mantiki na ushawishi katika kuigiza usaili wa nafasi ya kazi husika.
Shughuli ya 5.12 (c)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha
hoja zenye mantiki na ushawishi wakati wa kuigiza kama
mgombea wa nafasi ya uongozi katika uchaguzi wa shuleni.
Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika
kuandaa usaili wa kazi atakayoichagua na kuchukua nukuu.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya na kusahihisha kazi za
wanafunzi ili kuondoa upungufu unaojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.12 (c) yatategemea uelewa wa mwanafunzi
kwa kuzingatia nafasi ya kazi ambayo mwanafunzi ataichagua. Katika
uchambuzi, mwanafunzi aoneshe namna atakavyowasilisha hoja zenye
mantiki na ushawishi katika kuigiza usaili wa nafasi ya uongozi.
Somo la 6: Maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja zenye mantiki
na ushawishi katika malumbano ya hoja
Shughuli ya 5.13
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.13 iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
Kiongozi cha Mwalimu 67
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 67 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 67