Page 79 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 79
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 6.2 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano fursa zinazochochea
utunzi wa kazi za kifasihi.
FOR ONLINE READING ONLY
Somo la 3: Mchango wa TEHAMA katika kutambua fursa
zinazotokana na kazi za kifasihi
Shughuli ya 6.3
Hatua za ufundishaji
(i) Wauulize wanafunzi maswali kuhusu dhana ya TEHAMA,
majukwaa ya kidijiti, na jinsi ya kutumia majukwaa hayo.
Wanafunzi wajibu maswali hayo kutokana na uelewa wao.
Rekebisha majibu yao kwa kuelekeza namna ya kutumia
majukwaa hayo.
(ii) Waelekeze wanafunzi kupakua, kusoma na kueleza mchango
wa TEHAMA katika kutambua fursa zinazotokana na kazi
za kifasihi kama shughuli ya 6.3 iliyomo kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kuandaa malumbano ya hoja kuhusu
mchango wa TEHAMA katika kutambua fursa zinazotokana na
kazi za kifasihi, kisha hamasisha kila mwanafunzi kushiriki.
(iv) Waelekeze wanafunzi kuandaa uwasilishaji ambao utachagiza
kila mwanafunzi kushiriki kwa kutoa mchango na kuuliza
maswali ili kulifanya darasa kuwa changamshi, huku
ukiwasahihisha na kuondoa dosari zinazojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 6.3 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Majibu yanaweza hatua za kuandaa na kuchapisha kazi za kifasihi
Kiongozi cha Mwalimu 73
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 73 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 73