Page 84 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 84

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 6.8
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kubainisha masuala mtambuka kwa njia
           FOR ONLINE READING ONLY
                  ya bungua bongo.
             (ii)  Wagawe wanafunzi katika vikundi, kisha watunge igizo fupi kwa
                  kufuata kanuni za utunzi. Kila kikundi kitachagua mada moja
                  na kuiumbia visa na matukio, kisha waoneshe walivyozingatia
                  kila hatua na kanuni za utunzi wa igizo hilo.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kuwasilisha matini ya igizo kwa kuonesha
                  kila hatua na uzingativu wa kanuni za utunzi wa igizo lake.
                  Chagua vikundi vichache, viwasilishe huku wanafunzi wengine
                  wakisikiliza  na kuchangia  mawazo  yao pamoja  na kuuliza
                  maswali  kuhusu kile  kinachowasilishwa.  Rekebisha  dosari
                  zinazojitokeza.

           Majibu

           Majibu ya shughuli 6.8 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
           utunzi, mwanafunzi azingatie hatua na kanuni za utunzi wa maigizo.


             Somo la 6: Kanuni za utunzi na kutunga mashairi


           Shughuli ya 6.9
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 6.9 iliyomo kwenye
                  Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi  kusoma  vyanzo  mbalimbali  kuhusu
                  kanuni  zinazoongoza  utunzi  wa mashairi,  kuuliza  maswali,
                  kupima  uelewa  wa wanafunzi  kuhusu kanuni  za  utunzi  wa
                  mashairi na kueleza namna zinavyozitumika katika utunzi.



             78                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   78
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   78    23/06/2024   17:48
   79   80   81   82   83   84   85   86   87   88