Page 86 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 86

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari




             Somo la 7:  Kanuni za utunzi wa kutunga hadithi za watoto


           Shughuli ya 6.11 (a) na (b)
           FOR ONLINE READING ONLY
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kueleza kuhusu  dhana ya hadithi za
                  watoto.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukusanya vitabu vya hadithi mbalimbali
                  za watoto, kisha vigawe katika makundi kwa kufuata umri
                  na hatua za usomaji. Wagawe wanafunzi katika vikundi kwa
                  kufuata idadi ya makundi ya vitabu, wachambue sifa na kanuni
                  za utunzi wa hadithi zilizomo katika vitabu hivyo.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi walivyounda kujadili
                  sifa na kanuni za hadithi za watoto. Hakikisha kila mwanafunzi
                  anashiriki katika kutoa mawazo yake. Tembelea kila kikundi ili
                  kurekebisha dosari zinazojitokeza katika majadiliano.

             (iv)  Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji, kila kikundi
                  kichague mwakilishi awasilishe kazi yao na wanafunzi wengine
                  washiriki kwa kuchangia hoja na kuuliza maswali. Rekebisha
                  dosari zinazojitokeza katika uwasilishaji.

           Majibu

           Majibu ya shughuli 6.11(a) na (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Pia, yanaweza kuwa yale yaliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
           Mwanafunzi aeleze  upekee  wa utungaji  wa hadithi  za watoto
           unavyotofautiana na utunzi wa hadithi za watu wazima.











             80                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   80    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   80
   81   82   83   84   85   86   87   88