Page 65 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 65

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari



             Somo la 3: Maana zinazopatikana katika matini za kifasihi


           Shughuli ya 5.5 (a) na (b)
           FOR ONLINE READING ONLY
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kufanya  shughuli  ya  5.5 (a)  na  (b)
                  zilizomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi vya watu wasiozidi
                  wanne kujadili shughuli ya 5.5 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha
                  Mwanafunzi,  kisha jibu  maswali  yaliyotolewa  yanayotokana
                  na insha watayoijadili.  Pia,  kuchambua  maana  mbalimbali
                  zinazopatikana katika insha kwenye shughuli 5.5 (b). Hakikisha
                  kila mwanafunzi anatoa mawazo yake. Rekebisha dosari pale
                  zitakapojitokeza.

             (iii)  Waongoze  wanafunzi kuandaa  uwasilishaji,  chagua kila
                  kikundi kujibu swali moja kutoka katika shughuli ya 5.5 (a)
                  ili kuwasilisha kwa darasa zima. Pia, chagua vikundi kadhaa
                  kuwasilisha maana zilizopatikana  katika shughuli 5.5(b).
                  Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kwa kutoa mchango au
                  kuuliza maswali. Sahihisha upungufu unaojitokeza.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 5.5 (a) na (b) yatatokana na uelewa wa
           mwanafunzi. Katika shughuli hizi mwanafunzi atachambua  maana
           mbalimbali zinazopatikana katika insha hizo.

           Shughuli ya 5.6 (a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.6 (a) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.



                 Kiongozi cha Mwalimu                                    59
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   59    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   59
   60   61   62   63   64   65   66   67   68   69   70