Page 60 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 60

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


               (f)  Kutathmini kazi za fasihi kwa kutumia misingi ya ujenzi wa
                    hoja zenye mantiki na ushawishi; na

               (g)  Kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi kwa kutumia
                    maarifa ya kifasihi.
           FOR ONLINE READING ONLY
           Mahitaji

           Matini na makala za kifasihi, magazeti, hadithi, nyimbo, mashairi na
           maigizo yaliyorekodiwa, vitabu teule, kamusi na vinginevyo.


             Somo la 1: Vigezo vya ujenzi wa ujumi katika kazi za fasihi


           Shughuli ya 5.1

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kusikiliza au kutazama video za nyimbo
                  tano (5) ambazo anadhani ni nzuri na zingine tano (5) ambazo
                  anadhani ni mbaya kama inavyoelekezwa katika shughuli ya
                  5.1 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waongoze wanafunzi kuchambua maudhui ya nyimbo hizo
                  kisha kueleza sababu za nyimbo hizo kuwa au nzuri au mbaya.
                  Ongoza mjadala kisha rekebisha upungufu unaojitokeza.

           Majibu

           Majibu ya shughuli 5.1 yatategemeana  na uelewa wa mwanafunzi.
           Mwanafunzi ajibu kulingana nyimbo atakazozichagua.

           Shughuli ya 5.2 (a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kukaa  katika  vikundi  kujadili  shughuli
                  ya 5.2 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha




             54                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   54
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   54    23/06/2024   17:48
   55   56   57   58   59   60   61   62   63   64   65