Page 56 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 56

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 4.15(b)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kukaa katika  jozi  au vinginevyo
           FOR ONLINE READING ONLY
                  kujadiliana  shughuli ya 4.15(b) iliyomo  kwenye Kitabu cha
                  Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi  kufanya uwasilishaji  kisha, chagua
                  wanafunzi  wachache  kuwasilisha  kazi  zao darasani kwa
                  majadiliano zaidi huku ukirekebisha upungufu unaojitokeza.

             (iii)  Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusu shughuli husika.

           Majibu
           Majibu ya shughuli ya 4.15(b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua  athari za kiimani  na
           mitazamo katika nyimbo mbili za bongo fleva atakazozichambua.


           Shughuli ya 4.16(a)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandaoni au
                  vinginevyo kupakua na kusikiliza nyimbo mbalimbali za bongo
                  fleva, kisha kufanya kazi binafsi ya shughuli ya 4.16 (a) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Unaweza kuchagua wanafunzi wachache kuwasilisha kazi zao
                  au vinginevyo, hakikisha ushiriki wa kila mwanafunzi wakati
                  wa uwasilishaji. Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa
                  uwasilishaji
             (iii)  Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
                  husika.







             50                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   50
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   50    23/06/2024   17:48
   51   52   53   54   55   56   57   58   59   60   61