Page 52 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 52
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.11(b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo iliyomo
FOR ONLINE READING ONLY
katika tamthiliya teule mbili.
Somo la 4: Kuhusianisha mitazamo iliyomo katika bongo fleva,
mashairi na tamthiliya na matendo ya jamii
Shughuli ya 4.12(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mkondoni au
vinginevyo kupakua na kusikiliza au kutazama video za nyimbo
za bongo fleva, kisha kukaa katika vikundi kujadili shughuli ya
4.12 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kuwasilisha kazi waliyoifanya, hakikisha
ushiriki wa kila kikundi wakati wa uwasilishaji. Rekebisha
upungufu unaojitokeza.
(iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
waliyoiwasilisha.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.12 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo ya nyimbo za
bongo fleva atakazokuwa amezichambua.
Shughuli ya 4.12(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vifaa vya TEHAMA kupakua na
kusikiliza au kutazama video za nyimbo za bongo fleva katika
46 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 46 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 46