Page 47 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 47
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
ya 4.7(a) ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 4.7 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi alinganishe maadili na masuala ya
kiimani yaliyomo katika kazi hizo.
Shughuli ya 4.7(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.7 (b) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kusoma diwani mbili teule, kisha
wachambue maadili yaliyomo. Baadaye waandae matini ya
uchambuzi na kuikusanya kwa ajili ya maboresho.
(iii) Sahihisha kazi ya kila mwanafunzi ili kuondoa dosari
zinazojitokeza na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.7 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha maadili
yaliyomo na imani za jamii katika mashairi mawili ya diwani teule.
Shughuli ya 4.8(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma matini fupi ya tamthiliya iliyomo
kwenye shughuli ya 4.8(a) katika Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
kujadiliana katika vikundi kwa kujibu maswali yaliyotolewa.
(ii) Waelekeze wanafunzi kuandaa uwasilishaji, kisha chagua
wanafunzi wachache wawasilishe kazi zao kwa niaba ya
Kiongozi cha Mwalimu 41
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 41 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 41