Page 44 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 44

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


             (ii)  Waelekeze  wanafunzi kukaa katika kikundi cha wanafunzi
                  wasiozidi wanne, kisha wachambue maadili yaliyomo katika
                  tamthiliya mbili teule.

             (iii)  Waongoze  wanafunzi  kuwasilisha  maadili  yaliyomo katika
           FOR ONLINE READING ONLY
                  tamthiliya teule, kisha chagua vikundi vichache ili viwasilishe
                  kazi zao. Hakikisha kila mwanafunzi  anashiriki  kikamilifu
                  kisha kusanya kazi za wanafunzi.

             (iv)  Sahihisha kazi ya kila mwanafunzi ili kuondoa dosari
                  zinazojitokeza na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.
           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.4 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili yaliyomo katika
           tamthiliya teule.

           Shughuli ya 4.4(c)

           Hatua za ufundishaji
             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.4 (c) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi  kukaa  katika  vikundi  ili  kupakua  na
                  kusikiliza tamthiliya mbili kisha kuchambua maadili yaliyomo
                  katika  tamthiliya  hizo mbili  zinazorushwa  katika  vituo  vya
                  runinga.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kuwasilisha kwa kuchagua wanafunzi
                  wachache kuwasilisha kwa niaba ya wengine. Hakikisha kila
                  mwanafunzi anashiriki kikamilifu wakati wa uwasilishaji.

             (iv)  Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.4 (c) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atatumia mifano kuchambua maadili
           yaliyomo katika tamthiliya hizo mbili.


             38                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   38
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   38    23/06/2024   17:48
   39   40   41   42   43   44   45   46   47   48   49