Page 45 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 45
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 2: Ulinganisho wa maadili yaliyomo katika kazi za
fasihi na imani za jamii
Shughuli ya 4.5
FOR ONLINE READING ONLY
Hatua za ufundishaji
(i) Kwa njia ya bungua bongo, waongoze wanafunzi kubainisha
imani zilizomo katika jamii.
(ii) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali kusoma kazi
nne za ushairi na nne za tamthiliya kisha kukaa katika vikundi
ili kuchambua masuala ya kiimani yaliyomo katika kazi
hizo. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika
majadiliano na kutoa mawazo yake wakati wa uwasilishaji.
(iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusu shughuli ya 4.5
ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.5 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi atachambua masuala ya kiimani yaliyomo
katika kazi hizo kulingana na jamii yake.
Shughuli ya 4.6 (a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali kupakua na
kusikiliza nyimbo zinazohusiana na shughuli ya 4.6 (a) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi na kufanya shughuli
ya 4.6 (a) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi kisha
wakusanye kazi zao.
(iii) Sahihisha na toa mrejesho ili kuleta uelewa wa pamoja.
Kiongozi cha Mwalimu 39
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 39 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 39