Page 40 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 40

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


               (d)  Kuhusianisha mitazamo  iliyomo  katika  nyimbo  za  bongo
                    fleva, mashairi na tamthiliya na matendo ya jamii ; na

               (e)  Kujadili namna athari za kiimani na kimitazamo katika bongo
                    fleva, mashairi na tamthiliya zinavyojidhihirisha katika jamii.
           FOR ONLINE READING ONLY
           Mahitaji:  Matini na makala za kifasihi, magazeti, nyimbo za bongo
                     fleva, mashairi na tamthiliya zilizorekodiwa, vitabu teule, na
                     chati ya alama za LAT.



             Somo la 1:  Maadili katika nyimbo za bongo fleva, mashairi na
                        tamthiliya


           Shughuli ya 4.1

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kutumia vifaa vya TEHAMA kupakua na
                  kusikiliza au kutazama wimbo mmoja ambao unaona kuwa una
                  maadili na mwingine ambao hauna maadili kisha kukaa katika
                  jozi na kujadili shughuli ya 4.1 iliyomo kwenye Kitabu cha
                  Mwanafunzi.

             (ii)  Waongoze  wanafunzi  kuandaa  uwasilishaji  kwa kuchagua
                  wanafunzi  wachache  kuwasilisha kazi  zao na wengine
                  washiriki kwa kuuliza maswali na kuchangia hoja. Rekebisha
                  upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji ili kuleta uelewa
                  wa pamoja.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.1 yatatokana  na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika  shughuli hii, mwanafunzi  atachambua  sababu za  wimbo huo
           mmoja kuwa na mwingine kukosa maadili.







             34                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   34    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   34
   35   36   37   38   39   40   41   42   43   44   45