Page 38 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 38
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 7: Kutathmini mchango wa nadharia teule za uhakiki
wa kazi za fasihi katika maendeleo ya ushairi na
tamthiliya
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 3.17
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi visivyozidi
wanafunzi sita ili kufanya shughuli ya 3.17 iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi kisha kuwasilisha kazi zao darasani
kwa majadiliano zaidi huku ukirekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa majadiliano ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.17 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi atachagua utanzu wa ushairi au tamthiliya,
kisha kueleza namna nadharia za umaksi na mwingilianomatini
zinavyochangia katika maendeleo na uhakiki wa tanzu hizo.
(i) Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi ili kufanya zoezi la 3.4
lililomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kusanya kazi za
wanafunzi, sahihisha na kutoa mrejesho.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi kufanya maswali ya
tamrini yaliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(iii) Sahihisha na toa mrejesho kuhusiana na shughuli husika kwa
wakati.
Majibu
Majibu ya zoezi la 3.4 na maswali ya tamrini yatatokana na uelewa wa
mwanafunzi. Mwanafunzi ajibu kulingana na mahitaji ya swali husika.
Pia, hakikisha mwanafunzi anahusisha maarifa na maisha yake ya kila
siku.
32 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 32 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 32