Page 34 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 34

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


                  hakikisha kila mwanafunzi anashiriki katika uwasilishaji.
                  Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji.

           Majibu

           FOR ONLINE READING ONLY
           Majibu  ya  shughuli  ya  3.11 yatatokana  na  uelewa  wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze maana na misingi ya nadharia
           ya mwingilianomatini katika kuhakiki kazi za kifasihi.

           Shughuli ya 3.12

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Tumia  mbinu  ya  fikiri-jozisha-shirikisha,  kisha  waongoze
                  wanafunzi kufikiri, kisha waelezane mawazo yao katika jozi.
                  Baada ya kuyaunganisha mawazo ya jozi, kila jozi iwasilishe
                  mawazo yao darasani.

             (ii)  Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa uwasilishaji wa
                  majibu ya shughuli ya 3.12.

           Majibu

           Majibu  ya  shughuli  ya  3.12  yatatokana  na  uelewa  wa  mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze  kwa mifano sifa na dhima
           za mhakiki wa kazi za kifasihi. Pia, mwanafunzi aoneshe athari hasi
           za kutokuwa na mhakiki wa kazi za kifasihi ili kupata mitazamo
           mbalimbali.

             (i)   Waelekeze  wanafunzi kufanya zoezi la 3.2 lililomo kwenye
                  Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kusanya, sahihisha na toa
                  mrejesho.












             28                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   28
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   28    23/06/2024   17:48
   29   30   31   32   33   34   35   36   37   38   39