Page 31 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 31
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 5: Uchambuzi wa nadharia teule za uhakiki wa kazi za
fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 3.5
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi visivyozidi
wanafunzi wanne ili kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au
maktabani, wajadili shughuli ya 3.5 iliyomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya matembezi msambao ili
kujifunza katika majibu ya vikundi mbalimbali, hakikisha kila
mwanafunzi anashiriki kikamilifu.
(iii) Waongoze wanafunzi kuhitimisha majadiliano kwa kutoa
maarifa sahihi.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.5 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi aorodheshe nadharia kumi (10) za uhakiki wa
kazi za kifasihi.
Shughuli ya 3.6
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kuchunguza ramani ya dhana, kisha kwa
njia ya maswali na majibu, wafafanue maana na misingi ya
nadharia ya uumundo.
(ii) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili shughuli
ya 3.6 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kufanya
uwasilishaji. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu
ili kuchochea majadiliano.
Kiongozi cha Mwalimu 25
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 25 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 25