Page 27 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 27

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Mahitaji:  Chati/mti  wenye vipengele  vya fani na maudhui
                     yaliyorekodiwa na matini na makala za kifasihi, magazeti,
                     maigizo,  mashairi  na  tamthiliya  zilizorekodiwa,  kamusi,
                     vitabu teule, chati ya alama za LAT
           FOR ONLINE READING ONLY

             Somo la 1: Mtazamo kuhusu fani na maudhui


           Shughuli ya 3.1
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kukaa katika jozi, wakitafakari mitazamo
                  kuhusu fani na maudhui.

             (ii)  Waongoze wanafunzi kuwasilisha darasani mawazo yao
                  kuhusiana na mitazamo hiyo kwa njia ya kushindanisha jozi.

             (iii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi ili kujadili shughuli
                  ya 3.1 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha kila
                  mwanafunzi anashiriki kikamilifu.

             (iv)  Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji. Chagua baadhi ya
                  vikundi kuwasilisha kwa niaba ya vingine. Zingatia ushiriki
                  wa kila  kikundi wakati  wa uwasilishaji  wa kazi  za vikundi.
                  Rekebisha upungufu unaojitokeza  wakati wa uwasilishaji ili
                  kuwa na uelewa wa pamoja.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 3.1 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
           shughuli hii, mwanafunzi ajikite katika mitazamo miwili yaani kidhanifu
           na kiyakinifu. Katika mtazamo wa kidhanifu mwanafunzi aeleze namna
           vipengele  vya  fani  na  maudhui  vinavyoweza  kutenganishwa.  Pia,
           mtazamo wa kiyakinifu mwanafunzi aeleze namna vipengele vya fani
           na maudhui haviwezi kutenganishwa.





                 Kiongozi cha Mwalimu                                    21
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   21    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   21
   22   23   24   25   26   27   28   29   30   31   32