Page 23 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 23
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(iii) Waongoze wanafunzi kurekebisha upungufu unaojitokeza
katika mdahalo huo ili kuleta uelewa wa pamoja.
Majibu
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu ya shughuli ya 2.17 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze kwa mifano namna fasihi
simulizi ilivyochangia kupatikana kwa fasihi andishi.
Somo la 4: Athari za sayansi na teknolojia katika maendeleo ya
fasihi simulizi na fasihi andishi
Shughuli ya 2.18
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kuangalia au kusikiliza vipindi
mbalimbali vinavyohusiana na fasihi simulizi vilivyorekodiwa
au vinavyorushwa, kisha wakae katika jozi ili kufanya shughuli
ya 2.18 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waelekeze wanafunzi kuandaa kazimradi inayohusu athari za
sayansi na teknolojia katika maendeleo ya fasihi simulizi na
fasihi andishi. Katika majadiliano, sisitiza matumizi ya mifano
ili kuthibitisha hoja zinazotolewa. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki kikamilifu na kuchukua nukuu. Hakikisha
unahitimisha majadiliano hayo.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.18 na yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze athari zinazotokana na vipindi
hivyo kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari.
Kiongozi cha Mwalimu 17
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 17 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 17