Page 19 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 19

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 2.10
           Hatua za ufundishaji
             (i)   Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandoni na
                  maktabani katika jozi au vikundi ili kufanya shughuli ya 2.10
           FOR ONLINE READING ONLY
                  iliyomo  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi kisha wawasilishe
                  darasani  kwa majadiliano  zaidi.  Hakikisha kila  mwanafunzi
                  anashiriki katika uwasilishaji. Rekebisha upungufu unaojitokeza
                  ili kuleta uelewa wa pamoja.

           Majibu

           Majibu  ya  shughuli  ya  2.10  yatatokana  na  uelewa  wa  mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi aeleze dhana na historia ya hadithi
           fupi ya Kiswahili.


           Shughuli ya 2.11

           Hatua za ufundishaji
             (i)   Waongoze  wanafunzi  kutumia  vyanzo mbalimbali kufanya
                  shughuli binafsi  ya 2.11 iliyomo  kwenye Kitabu cha
                  Mwanafunzi. Kila mwanafunzi ashiriki kufanya kazi binafsi.

             (ii)  Unaweza kuwaelekeza wanafunzi kutumia njia ya changanya-
                  kete  ili  kuchagua  wanafunzi  wachache  kuwasilisha hadithi
                  zao walizosoma na kuzichambua. Hakikisha kila mwanafunzi
                  anashiriki kwa kuchangia mawazo yake na kuwauliza maswali
                  ili kuchochea majadiliano.

           Majibu
           Majibu  ya  shughuli  ya  2.11 yatatokana  na  uelewa  wa mwanafunzi.
           Katika  shughuli  hii,  mwanafunzi  abainishe  aina  za hadithi  fupi na
           kuchambua maudhui yaliyomo katika hadithi hizo.







                 Kiongozi cha Mwalimu                                    13
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   13    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   13
   14   15   16   17   18   19   20   21   22   23   24