Page 16 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 16
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 2.5
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya kazi binafsi kutokana na
FOR ONLINE READING ONLY
shughuli ya 2.5 (a) na (b) zilizomo kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi, kisha kukusanya kwa ajili ya kusahihisha na
kutoa maboresho ya kazi ya kila mwanafunzi.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.5 (a) na (b) yatatokana na uelewa wa
mwanafunzi. Mwanafunzi azingatie hatua na kanuni za utunzi
kulingana na kipera atakachokichagua. Pia, katika utunzi wa jigambo
mwanafunzi azingatie kanuni za utunzi wa majigambo na kuweka
ushikamani wa mada husika.
Shughuli ya 2.6
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kujadili
shughuli ya 2.6 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
kisha wawasilishe darasani. Hakikisha kila mwanafunzi
anashiriki kikamilifu katika uwasilishaji na rekebisha
upungufu unaojitokeza.
(ii) Hitimisha shughuli kwa kutoa mrejesho wa shughuli hiyo.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.6 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi afafanue kwa mifano maana, sifa na
aina za sanaa za maonesho. Mwanafunzi aeleze kwa ubayana namna
sanaa za maonesho zinavyoweza kutofautiana na kazi zingine za
kifasihi au kisanaa.
10 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 10
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 10 23/06/2024 17:48