Page 12 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 12

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari





               Sura ya

                  Pili            Fasihi simulizi na fasihi andishi






                         Utangulizi
            Katika sura hii, mwanafunzi atajifunza kuhusu tanzu na vipera vya
            fasihi simulizi na fasihi andishi. Pia, atajifunza namna ya kuhusianisha
            fasihi simulizi na fasihi andishi.  Aidha, atajifunza kuhusu mchango
            wa fasihi simulizi katika maendeleo ya fasihi andishi na mchango wa
            fasihi simulizi na fasihi andishi katika maendeleo ya jamii. Baada ya
            kujifunza, ataweza kuchambua na kutunga kazi za kifasihi kulingana
            na  tanzu na  kipera  husika.  Mwalimu  utapata  baadhi  ya  mbinu
            zitakazokuwezesha katika ujenzi wa umahiri huu kwa mwanafunzi.
             FOR ONLINE READING ONLY



                             Shughuli za kutendwa na mwanafunzi



           (a)  Kufafanua tanzu na vipera vya fasihi simulizi na fasihi andishi
           (b)  Kujadili uhusiano wa fasihi simulizi na fasihi andishi

           (c)  Kueleza mchango wa fasihi simulizi katika maendeleo ya fasihi
                andishi

           (d)  Kutathmini athari za sayansi na teknolojia katika maendeleo ya
                fasihi simulizi na andishi

           (e)  Kujadili  mchango wa fasihi simulizi  na fasihi andishi katika
                maendeleo ya jamii
           (f)  Kuhusianisha fasihi simulizi na fasihi andishi



              6                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   6
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   6     23/06/2024   17:48
   7   8   9   10   11   12   13   14   15   16   17